Tuna mifumo na kanuni za usalama za kukufanya uwe salama unapotumia huduma za kibenki kwa njia ya mtandao, kukulinda dhidi ya wizi wa taarifa zako au vihatarishi vingine. Soma kuhusu mikakati yetu na kile unachopaswa kufanya ili kubaki kuwa salama.

eggs in a nest

Tunachokifanya kwa ajili yako

Huduma za Kibenki kwa Njia ya Mtandao zinazotolewa na NBC zinatumia mbinu za kiteknolojia za hali ya juu ambazo zinakupatia uhakika wa usalama kwa kiwango cha juu.

  • Usalama wa Huduma za NBC Online Banking

    Mifumo ya usalama inajumuisha programu za firewall, mifumo ya kugundua, programu za kudhibiti virusi na nyingine nyingi. Kanuni za usalama zimepimwa na kuhakikishwa na makampuni ya uhakiki wa viwango ya kimataifa kwa kutumia viwango na utendaji unaokubalika kimataifa.

    Huduma za kibenki kwa njia ya mtandao zinatumia mfumo wa kuficha (encryption) taarifa za mteja anapotumia huduma za NBC Online Banking kuhakikisha mawasiliano ya wateja na benki kwa njia ya mtandao yanakuwa salama. Mbali na hizi mbinu za kiteknolojia, usalama pia huwekwa wakati wa mchakato wa kufungua akaunti ya mtandaoni. Huduma za Kibenki kwa Njia ya Mtandao hulazimisha kuingiza namba ya siri yenye jumla ya alama 8, zikiwamo namba na herufi (yaani alama za namba na herufi) na alama nyingine maalum. Huwa tunatumia pia maswali na majibu ya siri katika kuhakikisha usalama wa taarifa zako kwenye Huduma za Kibenki kwa Njia ya mtandao.

  • Namba ya Siri ya Kuingiza Mara moja tu (OTP)

    Unapoingiza namba ya mtu unayemtumia fedha au kwa ajili ya kulipia bili, unapohamisha fedha mara moja tu, au unapofanya miamala muhimu, namba ya siri ya kutumika mara moja tu (OTP) itatumwa kwenye simu yako ya mkononi. Unapaswa kuiingiza namba hii kwenye kijisehemu kitakachojitokeza kwa ajili ya uthibitisho. Namba hizi zitatumika mara moja tu, na hii inasaidia kupunguza hatari za kuibiwa.

  • Kutolewa mtandaoni (Timed logout)

    Huduma za kibenki mtandaoni hukutoa mtandaoni kama usipoitumia ndani ya dakika 5 baada ya kuingia (login). Hii huongeza usalama kama ulisahau kutoka mwenyewe mtandaoni baada ya kutumia.

  • Kushindwa kuingiza namba ya siri kwa usahihi mara tatu hukufanya ufungiwe akaunti yako kwa muda

    Kama namba ya siri au namba ya utambulisho isiyo sahihi itaingizwa mara tatu mfululizo, huduma za kibenki kwako kwa njia ya mtandao zitasitishwa kwa muda au zitafungwa na utatakiwa kutembelea tawi la NBC lililopo karibu au kupiga simu kwenye Kituo chetu cha Huduma kwa Wateja ili kutoa taarifa na kufanya utaratibu wa kukurudishia huduma hizo.

  • Kibodi Maalum

    Kibodi maalum zimeandaliwa kwa ajili ya kukusaidia kupunguza hatari za programu zinazojipakua zenyewe kwenye kompyuta na kuruhusu hali inayoweza kusababisha watu wengine kufikia akaunti yako. Kibodi maalum ni kifaa muhimu katika usalama wa huduma za kibenki kwa njia ya mtandao.

How we protect you

Unachopaswa kufanya

Wakati mtandao unaporahisisha mambo kwa kuwa na huduma za kibenki na manunuzi kwa njia ya mtandao, kuna hatari pia za usalama kwani wahalifu wanaweza kutumia mtandao kupata taarifa zako binafsi kama vile taarifa za kibenki na kutumia taarifa hizo kukuibia fedha zako.

  • Mambo muhimu ya kuzingatia ili kubaki salama

    • Epuka kutumia kompyuta zinazotumiwa na watu wengi unapotaka kutumia huduma za NBC Online Banking
    • Usifungue huduma za NBC Online Banking unapokuwa kwenye maeneo ya huduma za kompyuta (internet cafés), maktaba, au maeneo mengine ya jamii ili usihatarishe taarifa zako za kibeki kunakiliwa na kutumiwa baada ya wewe kuondoka eneo hilo
    • Badili namba za siri kila mara
    • Kama utahisi namba zako za siri zimeibiwa, piga simu mara moja NBC Huduma kwa wateja kwa namba +255 (0) 768 984 000, +255 (0) 222 193 000 or +255 (0) 225 511 000
    • Tumia namba ya siri kuingia kwenye kompyuta yako ili kudhibiti watu kuitumia kompyuta yako bila kibali chako
    • Zuia programu ya jaza kiatomati (auto complete) kwenye kivinjari cha kompyuta yako
    • Kumbuka siku zote kufunga huduma za NBC Online Banking na ufunge kabisa kivinjari hicho baada ya kukamilisha miamala yako
    • Kabla hujafanya miamala yoyote ya mtandaoni, hakikisha kwamba tovuti unayotumia iko salama. Mara unapofungua www.nbctz.com na kubofya kiungo cha Huduma za NBC Online Banking, utapelekwa moja kwa moja kwenye seva ya benki. Ukiwa hapo, angalia anuani ya kivinjari hicho. Hakikisha inaanza na ‘https://’ (Sio ‘http://’). Pia angalia kivinjari hicho kama kina sehemu ya kufungia na/au kufungulia – ambayo inapaswa kuwa juu au chini ya sikrini kompyuta yako
    • Weka programu nzuri ya usalama na hakikisha kwamba umeisasaisha (upgraded) kwenye matoleo mapya ya programu za kompyuta yako. Programu nyingi za kompyuta mpya zina uwezo wa kugundua na kudhibiti uhalifu wa mtandaoni
  • Baruapepe za udanganyifu (Phishing)

    • Baadhi ya wahalifu wanaweza mambo mengi makubwa ili kukuibia fedha zako – lakini kadiri unavyowagundua, ndivyo unavyopunguza uwezekano wa kuwindwa kwa njia ya intaneti au baruapepe za udanyanyifu (kuingiliwa)
    • Wezi wa mtandaoni mara nyingi hutuma baruapepe wakijidai wanatoka NBC (au mashirika mengine makubwa) – hii inajulikana kama ‘baruapepe za udanganyifu’ (phising). Baruapepe nyingi huonekana kama za kweli kwani hutumia nembo ya NBC na rangi za shirika ili kukushawishi kwamba baruapepe uliyopokea ni ya kweli
    • Mara nyingi, maudhui ya baruapepe hizo yanataja kwamba akaunti yako imefungwa kwa muda, na njia pekee ya kuirejesha ni kubofya kwenye kiunganisho wanachokupatia ili usasaishe taarifa zako. Japokuwa kiunganisho hicho hakikupeleki kwenye tovuti halisi ya NBC, tovuti hizo zimeandaliwa kwa ujanja ili zifanane na tovuti yetu, na hivyo inakuwa ngumu kuzitofautisha. Unapaswa kuwa makini kuhakikisha kwamba tovuti unayoingia ni tovuti halisi ya NBC

    Hapa chini kuna mfano wa b-pepe za udanganyifu:

    Mpendwa Mteja wa YYY bank,

    Baruapepe hii imetumwa kutoka kwenye seva ya Benki ya YYY ili kuhakiki baruapepe yako. Unapaswa ukamilishe mchakato huu kwa kibofya kiunganisho kilichopo hapa chini na kuingiza namba ya Kitambulisho chako cha YYY na namba ya siri kwenye kivinjari kidogo kitakachoonekana.

    Jambo hili linafanyika kwa usalama wako-kwa sababu baadhi ya wateja wetu hawatumii tena anuani zao za baruapepe na hivyo, lazima tuwahakiki. Ili kuhakiki baruapepe yako na kuweza kutumia akaunti yako, bofya kiunganisho kilichopo hapa chini:
    http://www.yyy.co.tz/wjwwU3gcnUhkTrqcR9AmuEvaPKkmvqsegOptMRPAqYof9UecGDV0xoNa3f0s3cz0a2

    Kiunganisho hiki kitakuunganisha moja kwa moja kwenye ukurasa wa waharifu kama inavyoonekana hapa chini:

    Wizi wa kuchelewa kidogo:
     
     
    Wakati fulani, wezi wa mtandaoni wanaweza kupata taarifa zako na kukaa nazo kwa muda mrefu kabla hawajafanya jaribio la kukuibia kwenye akaunti yako. Ni muhimu sana kubadili mara kwa mara namba za siri na za utambulisho unazotumia kuingia kwenye akaunti yako ili kuzuia wizi wa aina hii.
     
    Hatua za kufuata ili kuepukana na matatizo ya wizi wa udanganyifu:
    Japokuwa tuna njia mbalimbali za kukulinda usiibiwe, uelewa wako ni muhimu sana katika kuepukana na wizi wa udanganyifu wa kwenye mitandao; hivyo, zingatia yafuatayo unapopokea baruapepe inayodaiwa kutoka NBC:
     
    • Usijibu baruapepe hizi wala kubofya kwenye kiunganisho chochote
    • Usitoe taarifa za akaunti yako kama vile Namba ya Siri na taaifa nyingine za akaunti yako kwa njia ya baruapepe au kwenye kiunganisho cha baruapepe hizi. Sisi tayari tuna taarifa zote muhimu za akaunti yako kama vile Namba ya Kitambulisho, namba ya simu na anuani ya baruapepe na hatutakuomba taarifa hizi kwa njia ya baruapepe
    • Usijaribu kuingia kwenye tovuti yetu kwa kutumia kiunganisho chochote unachotumiwa kwenye baruapepe – siku zote tumia anuani yetu (www.nbc.co.tz )
    • Futa baruapepe taka zote mara moja unapoziona. Hata ombi linalokuja kukuomba kuondoa anuani ya baruapepe yako kwenye orodha fulani ya baruapepe inaweza kuwawathibitishia wezi wa mtandaoni kwamba anuani yako ya baruapepe  ni hai na inatumika, na hivyo inaweza kukuanika kwa wezi wengi zaidi
    • Usije ukafungua kiambatisho chochote cha baruapepe isipokuwa kama unajua aliyetuma ujumbe huo
    • Tumia vivinjari vya karibuni ambayo huja na vichuuja barua taka na vinahadharisha unapotembelea tovuti isiyo salama. NBC haitakutumia barua au b-pepe ikikuomba ujaze taarifa za akaunti yako kwa kubofya kiunganisho kwenye b-pepe
    • Tambua kwamba baruapepe za udanganyifu zimekuwa zikipokelewa pia kupitia Mazungumzo ya kwenye Google au Skype; pamoja na kwenye mitandao ya kijamii kama vile Facebook. Unapokuwa huna uhakikika na ukweli wa kiunganisho au madai fulani, ni bora usibofye kabisa
  • Kubadili Kadi ya Simu ya Mkononi

    Mhalifu anaweza kujaribu kubadili Kadi ya Simu yako ya mkononi kwa isivyo halali kupitia kwa mtoa huduma wa simu yako ya mkononi, mfano kwa kubeba nakala ya uongo ya kitambulisho chako. Hii inampa mhalifu nafasi ya kutumia kikamilifu akaunti ya simu yako ya mkononi na kupokea ujumbe wowote unaotumwa kwako. Watakuwa wanapokea pia taarifa za siri za akaunti yako ya benki na kufanyia kazi ujumbe wa simu ya mkononi unaotumwa kwa wateja. Kama tayari wameshakudanganya ukawapatia taarifa zako binafsi na taarifa za akaunti yako, wanaweza kuhamisha fedha kutoka kwenye akaunti yako bila wewe kujua.

    Unapaswa:

    • Unapaswa kutunza vizuri taarifa zako binafsi, za akaunti yako ya benki na za akaunti ya simu ya mkononi – hata unapokuwa mtandaoni
    • Unapaswa kuchunguza mara moja unapogundua kwamba hupokei ujumbe na simu unazopigiwa kwenye simu yako ya mkononi kama ilivyokawaida
    • Washa simu yako muda wote – vinginevyo hutagundua kama kadi ya simu yako imechezewa

Je, unahitaji taarifa au msaada zaidi?

Tupigie:

+255 768 984 000
+255 (0) 222 193 000
+255 (0) 225 511 000
0800711177 (free)

Tuandikie:

contact.centre@nbc.co.tz

Wasiliana nasiMatawi ya NBC