Kupitia uzoefu wa miaka zaidi ya 20, NBC inakupatia aina mbalimbali za bima kwa ajili ya watu wako na mali zako.
Bima nafuu kwa ajili ya gari lako
NBC inakupa uchaguzi wa bima ya gari inayokidhi mahitaji yako na kwa bei nafuu dhidi ya ajali, uharibifu, wizi na madai kutoka kwa wengine.
Kata bima NBC kwa ajili ya nyumba yako na vitu vya nyumbani kwako
Bima kwa ajili ya nyumba yako kuanzia kwenye sakafu hadi paa, nje na ndani, inayojumuisha vitu vya thamani vya nyumbani kwako.
Manufaa ya Bima ya Nyumba ya NBC
Ni bima kwa ajili ya:
- Uharibifu wa jengo
- Uharibifu wa samani mbalimbali zilizopo nyumbani kwako
- Upotevu unaotokana na moto au ujambazi
- Uharibifu au upotevu wa vitu vya ndani
Pia inahusisha:
- Bima ya Madeni
Ilinde familia yako kwa kukata Bima ya Maisha NBC
Katia bima samani za ndani ya nyumba yako dhidi ya hatari zozote. NBC Tunatoa bima za kifo, kupunguzwa kazini na ulemavu wa kudumu utokanao na ajali.
Tutakusaidia kuwa na bima kwa ajili ya familia yako
Kupitia huduma mbalimbali za bima zinazoambatanishwa na akaunti na mikopo ya NBC, zinakuwezesha kuishi kwa amani na furaha ukijua kwamba mkopo wako una bima itakayoilinda familia yako kama kutatokea lolote.
Je, unahitaji taarifa au msaada zaidi?
Tupigie
+255 76 898 4000 | +255 22 219 3000 | +255 22 551 1000 | 0800711177 (free)
Tuandikie baruapepe: