Ni rahisi sana kukimbia kwenye mashine ya ATM unapokuwa na hitaji la fedha, lakini mashine hizi zinakupa huduma nyingi zinazokurahisishia maisha katika kuweka fedha kwenye akaunti yoyote ya NBC, kufanya malipo ya ada za shule au chuo, kutuma fedha kwa mtu asiye na akaunti kabisa na kufanya manunuzi ya muda wa maongezi na mengine mengi.
Unaweza kufanya haya yote kwenye ATM ya NBC
Kuweka Fedha
Mashine ATM za NBC zilizopo matawini zinao uwezo wa kupokea fedha pale mtu yeyote anapotaka kuweka fedha taslimu kwenye akaunti yoyote ya NBC-Hata kama huna kadi ya ATM. Unachohitaji ni kuwa na namba ya akaunti tu. Hii inamaanisha:
- Fedha zinaweza kuwekwa moja kwa moja kwenye akaunti yako ya NBC
- Mtu anayeingizia fedha siyo lazima awe na akaunti NBC
- Unaweza kulipia kwa urahisi bidhaa au deni moja kwa moja kwa kuweka fedha kwenye akaunti ya NBC ya muhusika
- Unaweza kuweka fedha za mauzo yako ya kila siku kwenye akaunti yako ya NBC wakati wowote hata kama ni usiku
- Unaweza kutuma fedha kwa rafiki na jamaa zako popote kwa kuwawekea kwenye akaunti zao za NBC wakati wowote
- Mashine za ATM za NBC zipo wazi muda wote hata usiku wa manane
- Unapata risiti mara moja ikikuthibitishia fedha ulizoweka
- Aliyewekewa fedha atapokea ujumbe mfupi wa simu unaomtaarifu kiasi cha fedha kilichowekwa
- Unaweza kuangalia salio lako kwenye simu yako ya mkononi kupitia huduma za kibenki kwenye simu ya mkononi au huduma za kibenki mtandaoni
Kuongeza Salio la Simu
Mashine zetu za ATM zinakuwezesha kununua muda wa maongezi wa simu yako wakati wowote. Hii inamaanisha, mtu yeyote mwenye kadi ya ATM anaweza kununua muda wa maongezi wakati wowote bila kuwa na fedha taslimu.
Cash Popote
Je, unafahamu kwamba unaweza kutuma fedha kwa familia na marafiki hata kama unayemtumia akaunti ya benki yoyote? Halikadhalika, haihitaji kuwa na kadi ya benki ili uchukue fedha ulizomtumia. Unachopaswa kuwa nacho ni simu ya mkononi tu.
Unahitaji maelezo au msaada zaidi?
Wasiliana nasi:
+255 76 898 4000 | +255 22 219 3000 | +255 22 551 1000 | 0800711177 (free)
Tuandikie: