Benki ya Taifa ya Biashara inazingatia utunzaji siri wa taarifa za wateja wetu. Tunapozungumzia ‘taarifa za wateja wetu’ tunamaanisha taarifa zozote kuhusu mteja ambazo mteja mwenyewe au mtu mwingine ameziwasilisha kwetu.

 

Chaguo la mteja

Uamuzi wa mteaja kujipatia NBC taarifa zake kwa njia ya mtandao huwa ni chaguo la mteja mwenyewe. Hata hivyo, mteja anapaswa kujua kwamba miamala yoyote ya kifedha zinazozuia Baadhi ya taarifa inaweza kuipa NBC mipaka katika huduma tunazozitoa.

Saidia katika kulinda siri za mteja

Mteja pia anaweza kusaidia katika kudumisha usiri wa taarifa za kibenki kwa:

  • Kutomshirikisha mwingine kuhusiana na taarifa za Kitambulisho cha Mteja au namba yake ya siri
  • Kubadili namba ya siri ya mteja mara kwa mara
  • Kufunga akaunti kila mara anapofanya miamala ya kibenki kwa njia ya mtandao
  • Kutoacha kompyuta ya mteja bila mtu wakati wa kutekeleza miamala ya mtandaoni
  • Kutoa taarifa ya upotevu au kuibiwa kwa kadi
  • Kuisaidia benki ya NBC kuwa na kumbukumbu sahihi kwa kutoa taarifa kunapotokea mabadiliko yoyote kwa upande wa mteja ili waweza pia kusasaisha kumbukumbu zake
  • Kutotuma taarifa yoyote ya siri kupitia b-pepe isiyo na namba ya siri
  • Kutotoa taarifa yoyote ya binafsi na ya kifedha kwenye mazingira yoyote au kwa mtu yeyeyote ambaye humwamini
  • Kutofanya miamala wala kuwezesha miamala ya NBC kwa kutumia chombo kisicho na usalama (simu ya mkononi, mtandao, nk.)
Kulinda taarifa za mteja
  • Taarifa za mteja ni nini?
    Taarifa za mteja ni taarifa binafsi na za siri zinazomtambulisha au zinazohusiana naye ambazo hupelekwa NBC kupitia tovuti, mteja anaweza kuwa na mtu binafsi au biashara. Taarifa hizi zinahusisha jina, umri, namba za Kitambulisho, namba za usajili, anuani na mawasiliano mengine, utambulisho wa kijamii, jinsia, dini, madeni, taarifa za kipato na malipo, taarifa za fedha na taarifa za kibenki kama vile namba ya akaunti.
  • Kwa nini benki ya NBC hukusanya taarifa za mteja?
    Benki ya NBC hutumia taarifa za mteja ili kumtambua na kumpatia huduma bora za mtandaoni. Taarifa za mteja ni muhimu pia katika kuisaidia NBC kuwasiliana na mteja tunapokuwa na maswali yoyote. NBC pia hutumia taarifa za mteja ili kumfahamisha mteja juu ya huduma na bidhaa nyingine zinazotolewa na NBC. Hivyo, kadiri tunavyokufahamu vizuri, ndivyo tunavyoweza kukuhudumia vizuri pia.
  • Benki ya NBC inalindaje usalama wa taarifa zako?
    Kutunza kwa usalama taarifa zako za kifedha ni moja ya majukumu makuu ya NBC. Sera hii inaongoza hata mwenendo wa wafanyakazi katika masuala mazima ya usahihi, usiri na usalama wa taarifa zote za mteja.
Uwajibikaji katika kutoa taarifa za mteja

 Mazingira pekee ambayo NBC inaruhusiwa kutoa taarifa za mteja ni pale tu: unapoziomba wewe mwenyewe na pale inapolazimu katika kukuhudumia.

  • Kwa Idhini ya Mteja
    Benki ya NBC haitachukua wala kutumia taarifa ya mteja bila kupata idhini ya mteja mwenyewe.
    Katika mazingira ya kutangaza huduma au bidhaa zetu, tutahitaji idhini ya kukusanya au kutumia taarifa hiyo kwa maandishi (kwa mfano, kusaini mkataba) inapoonekana hivyo (mfano, kama mteja atapewa fursa ya kuchagua aina ya taarifa za kutoa, lakini akaamua kutozitoa, itaonekana kwamba mteja amechagua kutoa taarifa hizi).

    Aina ya taarifa atakazoombwa mteja zitatofautiana kulingana na aina ya bidhaa au huduma inayohitajika.

    Benki ya NBC ina vitengo vingi vya biashara.  Kutegemeana na mahitaji ya mteja na pale tu atakaporidhia, na kwamba kwa kushirikishana taarifa za mteja kati ya vitengo mbalimbali vya NBC inasaidia katika kumhudumia mteja kwa ufanisi.

    Makampuni mengine huwasiliana na Benki ya NBC kwa ajili ya mikopo na taarifa za kifedha. Hata hivyo, NBC hutoa taarifa hizo katika mazingira ambayo mteja mwenyewe ameomba au ameridhia kutolewa kwa taarifa hizo.

  • Kwa mujibu wa sheria
    Hii kwa kiasi kikubwa inahusiana na masharti ya taarifa za kodi za serikali au agizo la mahakama au pale inapohitajika kwa mujibu wa sheria au kulingana na sheria ya nchi. Hata hivyo, Benki ya NBC katika mazingira yoyote ya kisheria, itatoa taarifa mahsusi tu zilizoombwa.

  • Maslahi ya Umma
    Hii haitatumika kama sababu ya kutoa taarifa za mteja au akaunti ya mteja (ikiwamo jina na anuani) kwa mtu yeyote kwa madhumuni ya biashara. Hata hivyo, taratibu za kawaida zinazolinda maslahi ya NBC wakati mwingine hufanya taarifa za mteja zitolewe kwa mtu mwingine, mfano hundi inayorudishwa kutokana na upungufu wa fedha kwenye akaunti ya mteja.

  • Maslahi ya kijamii
    Wakati mwingine, NBC huombwa kutoa taarifa za mteja kwa maslahi ya kijamii, mfano taarifa za kusaidia kuzuia uharifu. Kabla ya kutekeleza maombi ya namna hii, NBC huchukua hadhari zote kuhakikisha kwamba mamlaka zote zinazohusika zina sababu za msingi za kuleta maombi hayo.

  • Wakala wa mikopo
    Taarifa kuhusu salio la mteja lililopo NBC linaweza kuelezwa kwa wakala wa mikopo aliyetambulishwa, pale ambapo mteja ametoa idhini ya maandishi kwa NBC kufanya hivyo. Benki ya NBC ina wajibu wa kutoa taarifa ya mikopo kila mwezi kuhusu mkopo huo kwa vyombo vyote vya mikopo vilivyopo na vitakavyoanzishwa.
Zana za Mipango

NBC haitunzi taarifa za mteja zinazotolewa kwenye program za mipango wanazotumia wateja (kwa mfano kukokotoa kiwango cha riba ya mkopo au ya akiba). Zana hizi ni kwa ajili ya kumsaidia mteja kufanya maamuzi yake ya kifedha kwa siri.

Haki ya kurekebisha sera ya usiri

NBC ina haki ya kurekebisha sera hii wakati wowote. Marekebisho yote kwenye sera hii yatawekwa kwenye tovuti. Isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo, toleo hili la sasa hivi linafuta matoleo mengine yote yaliyotangulia ya sera hii.

Matamko ya usiri yanayohusiana na huduma mahsusi za mtandaoni

Huduma mbalimbali zinazotolewa kwa njia ya mtandao, vitengo mbalimbali vya NBC vinaweza kuwa na sera zake za usiri kwa sababu aina ya huduma au bidhaa inalazimu kukiuka masharti ya sera hii. Sera hizo zitatumika tu kumwongoza mteja wa huduma au bidhaa hizo mahsusi za mtandaoni.

Watu wengine

Isipokuwa tu kama imetajwa kwenye sehemu ya "Utoaji wa Taarifa za Mteja", NBC haitauza wala kutoa taarifa za mteja kwa taasisi au mtu mwingine, zikiwamo kampuni.

Mawasiliano ya Beruapepe

NBC inaweza kutumia taariza za mteja kumtumia mteja huyo taarifa za huduma au bidhaa mpya ambazo anaweza kuzihitaji na wakati fulani kumtumia mteja ujumbe kwa njia ya posta, baruapepe au ujumbe kwa njia ya simu yake ya mkononi ili kumjulisha kuhusu bidhaa na huduma za NBC.

Mteja atakuwa na uchaguzi wa kueleza kwamba hahitaji kupokea ujumbe kama huo kwa siku za baadae, mara tu anapoona ujumbe huo. Hata hivyo, mteja ataendelea kupokea ujumbe kuhusu bidhaa nyingine mpaka hapo atakapochagua kutopokea taarifa za bidhaa hiyo tena.

Kumbuka kuwa upokeaji wa baruapepe zisizo na usiri si salama. Kwa mantiki hiyo, NBC haitaweka taarifa za siri za akaunti yako kwenye majibu ya baruapepe.

Aidha, NBC haitamuomba mteja kutoa taarifa binafsi kwa njia ya baruapepe, mfano namba ya akaunti, Namba ya Utambulisho BInafsi wala namba ya siri.

Maadili ya Kibenki

Benki ya NBC inaunga mkono na kusisitiza utekelezaji wa Maadili ya Kibenki.

Je, unahitaji taarifa au msaada zaidi?

Tupigie:

+255 768 984 000 | +255 (0) 222 193 000 | +255 (0) 225 511 000 | 0800711177 (free)

Tuandikie baruapepe:

contact.centre@nbc.co.tz

Wasiliana nasiTafuta tawi