Huduma za kijamii za NBC zimeendelea kukua na kuimarika miaka kadhaa iliyopita kutoka kwenye ajenda endelevu ya kujitolea zaidi inazingatia kuifikia jamii kwa upana. Mkabala wetu huu umeegemezwa katika nguzo tatu:

Elimu na ujuzi kwa vijana

Tunajitahidi kuwapatia vijana mafunzo ya ujuzi na maendeleo wanayoyatamani ili waweze kupata ajira rasmi au kujiajiri na kuwajiri wengine.

Maendeleo ya Ujasiriamali

Tunaamini kwamba kwa kuwawezesha wafanyabiashara ndogondogo na za kati tutakuwa tunasaidia kukuza uchumi wa taifa.

Jumuisho la Huduma na Kibenki

Lengo letu ni kuwawezesha watanzania wengi kupata na kutumia huduma za kibenki.

Tunawasaidia waweze kukua kutoka kuwa wanafunzi na kuwa wachapakazi

Kama benki ya taifa la wachapakazi, tunajitahidi kuwapa vijana ujuzi na maendeleo wanayohitaji ili waweze kupata ajira rasmi au kujiajiri, na pia kuwasaidia baadhi ya wanafunzi waweze kupata elimu ya juu.

Programu ya Wajibika

Wajibika ni programu inalenga kuwasaidia vijana wa Kitanzania wakuze ujuzi wa kufanya maamuzi na kubadili mtazamo kuhusiana na swala zima la ajira, watoke kutegemea tu kuajiriwa na waweze kuona fursa za kujiajiri. Mkakati huu unawapatia vijana mafunzo yanayowapa ujuzi na ufahamu wanaohitaji katika fursa za ajira.

Mkakati wa Wajibika unashughulikia kuziba pengo kubwa sana walilonalo vijana wanapohama kutoka kwenye maisha ya uanafunzi na kwenda katika maisha ya kufanya kazi. Kuziba pengo hili si tu kwamba kutawawezesha kuhamisha fikira kwa usahihi bali pia kutaongeza ufanisi katika kazi.

Mafunzo ya Wajibika hutolewa mtandaoni kupitia kiungo www.nbcwajibika.co.tz  kilichopo kwenye tovuti ya NBC, na pia hutolewa kupitia mafunzo ya ana kwa ana katika semina na washa zinazoendeshwa mara chache na NBC katika vyuo mbalimbali na kwenye shule za sekondari jijini Dar es Salaam.

Request for Proposal (RFP)

Jifunze zaidi

Programu za Udhamini wa Masomo

  • Hizi zitatolewa kwa wanafunzi wenye sifa ambao si wategemezi wa wafanyakazi wa NBC na ambao wanatoka katika familia zenye kipato cha chini na kwenye jamii duni, na kwa walemavu
  • Benki ya NBC inashirikiana na vyuo vya elimu ya juu nchini kuweza kufanikisha programu huu
  • Vyuo vitachagua wanafunzi wenye kukidhi vigezo vya kupata udhamini huu kutoka NBC, kwa kuzingatia taratibu zilizowekwa
  • Udhamini huu pia utaangalia viwango vya ufaulu vya wanafunzi
  • Fedha za udhamini zitalipwa moja kwa moja kwenye chuo anachosoma mwanafunzi

Tunawasaidia wafanyabishara wa kike na wa kiume kustawi

NBC B-Club ni Klabu ya biashara inayokusudiwa kuwalea Wafanyabiashara Ndogondogo na za Kati (SMEs) kupitia mafunzo katika masula ya ujasiriliamali, ujuzi wa fedha na ujuzi wa watu, taratibu na sheria za nchi kuhusu ufanyaji wa biashara. NBC B-Club inawapa njia ya kutatua changamoto zinazowakabili wanaume na wanawake wafanyabishara nchini.

 

Kupitia NBC B-Club, Wafanyabiashara Ndogondogo na za Kati wanapata fursa ya kushiriki warsha na maonesho mbalimbali ya kibiashara ndani na nje ya nchi,  kupata mafunzo kupitia mkakati wa ubia wa TANTRADE, TRA, TCCIA, SIDO na TIC.

Jifunze zaidi

Tunajali ukuaji na mfanikio ya kifedha ya watu wote

Lengo letu ni kuboresha huduma zetu za kibenki na kuanzisha mikakati inayowajumuishaji watu wengi zaidi kupata na kutumia huduma za kibenki kwa urahisi zaidi.

Huduma za Kibenki kwa ajili ya vijana

 

Tunawafikia vijana kupitia akaunti zetu za wanafunzi.

Jifunze zaidi

Huduma za Kibenki kwa vikundi vya kijamii

 

Tunatoa msaada kwa vikundi vya ndani kupitia Akaunti ya NBC Kikundi.

Jifunze zaidi

 

Je, wewe tayari ni mteja wa NBC? *

Zingatia: Vipengele vilivyowekewa nyote (*) ni vya lazima.

Unahitaji maelezo zaidi au msaada?

Tupigie:

+255 768 984 000 | +255 (0) 222 193 000 | +255 (0) 225 511 000

Tuandikie baruapepe:

 NBC_MarketingDepartment@nbc.co.tz

Wasiliana nasiMatawi ya NBC